Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa FAO/WHO wakutana kujadili kemikali ya BPA

Wataalamu wa FAO/WHO wakutana kujadili kemikali ya BPA

Shirika la afya duniani linandaa mkutano wa kisayansi wa kimataifa wa siku nne kujadili masuala ya afya na kemikali ya bisphenol A au BPA.

BPA ni kemikali ya viwandani inayotumika kutengeza vifaa ya plastiki vinavyotumiwa na wengi kama vile chupa za kulisha watoto wadogo, vyombo vya kuhifadhi chakula, chupa za maji maziwa na vinywaji vingine pamoja na mabomba ya maji.

BPA pia inatumika kwenye vyombo vya chuma vya kuhifadhi chakula na vinywaji. Mkutano huu unaandaliwa na WHO kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la chakula na mazoa FAO na kuungwa mkono na shirika la Health Canada.