Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

IOM inatoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Kituo cha shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa sasa kinasadia kutoa habari kwa waathiriwa wa mafuriko nchini Pakistan kuhusu ni wapi wanaweza kupata huduma za kibinadamu na jinsi ya kuzipata.

Tangu kituo hiki kianze kutoa huduma juma lililopita kimekuwa kikipokea kati ya siku 1000 na 1800 kwa siku.

Wengi wa wanaopiga simu kwenda kwa kituo hicho Wanataka kujua jinsi j ya kutibu maradhi ya Kidingapopo au homa ya vipindi ambayo kwa sasa imeathiri sehemu kadha nchini Pakistan na sana sana wakati huu. Wapiga simu wengine pia wanataka kufahamu jinsi wanaweza kujisajili ili wapate kufidiwa na serikali.