Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shughuli zimeanza kufungua barabara nchini DRC:IOM

Shughuli zimeanza kufungua barabara nchini DRC:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM juma hili linatarajiwa kuanzisha shughuli ya dharura ya kufunguliwa tena kwa barabara ya Dungu-Duru-Bitima nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya kutotumiwa kutokana na sababu za kuwa katika hali mbaya na ukosefu wa usalama.

Mradi huo wa dharura una lengo la kuifanya barabara hiyo iweze kutumika katika utoaji wa huduma za kibinadamu ifikapo Machi mwaka 2011. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

IOM imechukua hatua ya kuikarabati upya barabara hiyo ili kurahisha shughuli za upekekaji wa misaada nchini humo kuanzia March mwakani.Bara bara hiyo iliashwa kuhudumiwa kwa kipindi kirefu kwa sababu za kiusalama.

Bara bara hiyo yenye urefu wa kilometa 125 na kiungo muhimu cha kuunganisha maeneo ya Kaskazini kuanzia mji wa Dunga hadi karibu na mpaka wa Sudan. Eneo hilo lina watu zaidi ya 113,611 walio wakimbizi wa ndani ambao wanahitaji kufikiwa na huduma za kibinadamu.