Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yaweka mitambo kusaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

ITU yaweka mitambo kusaidia waathirika wa mafuriko Pakistan

Chama cha kimataifa cha mawasiliano kimepeleka mitambo 100 ya mawasiliano ya satellite kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini Pakistan.

Mitambo hiyo inawekwa ili kuwesesha kuwepo kwa mawasilino na utoaji wa huduma kwenye sehemu ambazo ni vigumu kufika na ambazo zinahitaji huduma za madawa baada ya janga mafuriko kuikumba Pakistan.

Karibu watu milioni 20 waliathiriwa na mafuriko hayo yanayotajwa kuwa mabaya zaidi katika historia ya Pakistan. Kwa sasa kuna changamoto nyingi zikiwemo za magonjwa yanayotokana na maji na utapiamlo wakati serikali na wafanyikazi wa kutoa misaada wakijaribu kutoa huduma za matibabu kwa waathirika.

Mitambo hiyo itarahisisha mawasiliano kati ya wafanyakazi wa kutoa huduma za mataibabu kwenye maeneo yaliyoathirika na mafuriko na vituo vilivyo mbali na pia ikiwa watahitaji kuomba ushauri kutoka kwa madaktari walio sehemu zingine za ulimwengu.