Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada yawafikia waathirika wa mafuriko Benin

Misaada yawafikia waathirika wa mafuriko Benin

Mashirika ya kibinadamu yanaendelea kutoa misaada kwa watu walioathirika na mafuriko nchini Benin wakati mvua bado zikiendelea kunyesha kote nchini na kufanya viwango vya mto Niger ulio kaskazini kupanda hadi kuzua wasiwasi.

Hadi sasa takriban watu 680,000 wameathirika na mafuriko hayo yaliyoanza kushuhudiwa mwezi Septemba. Watu wengine 200,000 kwa sasa wanahitaji makao baada ya zaidi ya nyumba 50,000 kuharibiwa , huku ekari 128,000 ya mazao ya kilimo ikiharibiwa na mifugo 81,000 kufariki.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Benin Nardos Bekele-Thomas anasema kuwa mahitaji ni mengi lakini watafanya wawezalo kuhakikisha kuwa hatua zinazohitajika zimechukuliwa kwa haraka. Flora Nducha na taarifa kamili.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)