Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubaguzi ni tatizo kwa kila jamii:Muigai

Ubaguzi ni tatizo kwa kila jamii:Muigai

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa kijamii na chuki kwa wageni amesema kuwa ubaguzi na chuki kwa wageni bado vimo miongoni mwa jamii na hakuna taifa linaloweza kudai kutoku na tatizo hilo.

Akiwasilisha ripoti kwa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Githu Muigai amesema ubaguzi na chuki kwa wageni bado yanasalia kuwa matatizo makubwa hadi leo.

Bwana Muigai amesema kuwa ikiwa mtu anasimishwa , kukaguliwa , kuhojiwa au kukamatawa kwa sababu ya dini yake au wakati muhamiaji ,mkimbizi au mtafuta hifadhi anapobaguliwa kila siku kwa kuwa yeye si mwananchi au wakati mcheza kabumbu anapokejeliwa kwa sababu ya rangi ya ngozi yake wote hao wanaonyesha kuwepo kwa tatizo hili.

Sasa muigai anaonya kuwa ubaguzi huu unaweza kusababisha kutokea kwa mauaji ya halaiki , uhalifu wa kivita, Vita vya kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu.