Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kimbunga Giri chasababisha maafa na uharibifu Myanmar

Kimbunga Giri chasababisha maafa na uharibifu Myanmar

Ripoti zinasema kuwa watu 45 wameaga dunia baada ya kimbunga Giri kuikumba Myanmar ambapo pia watu wengine 49 walijeruhiwa.

Watu wengine 10 hawajulikani waliko baada ya kimbunga hicho kusababisha watu 81,000 kubaki bila makao na takriban nyumba 15 kuharibiwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la mazao na kilimo FAO linakadiria kuwa zaidi ya ekari 40,000 za mchele zimeharibiwa.

Nayo mashule 430 na vituo vya afya 57 navyo vimeharibiwa na kimbunga hicho. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Kwa sasa serikali , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na ya Umoja wa Mataifa yanagawa misaada na kutoa huduma za matibabu kwenye miji iliyoathirika zaidi.