Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuwaomba wahisani msaada zaidi kusaidia bajeti ya OCHA

UM kuwaomba wahisani msaada zaidi kusaidia bajeti ya OCHA

Umoja wa Mataifa utawaomba wahisani kusaidia kwa kiasi kikubwa bajeti ya masuala ya kimbinadamu kwa mwaka ujao amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

Akizungumza mjini Geneva mkuu huyo Bi Valarie Amos amesema majanga yaliyoikumba Haiti na Pakistan yameiacha katika hali ngungu kifedha ofisi yake lakini anaimani ya kuendelea kupata msaada kutoka kwa serikali mbalimbali licha ya matatizo ya kifedha ambayo yamewaathiri wahisani wengi.

Bi Amos amesema Umoja wa Mataifa inatathimini njia mbadala na za kibunifu kuweza kuchangisha fedha zikiwemo za kushirikisha sekta binafsi kufadhili operesheni za dharura.

(SAUTI VALARIE AMOS)

"Lazima tuwe yakinifu na kitakachotokea , na kama ukiangalia idadi ya maombi tuliyozindua kwa mwaka jana , ni zaidi ya asilimia 50 tuu ndio yaliyofadhiliwa. Hivyo nitawaomba nchi wanachama kujitoa zaidi lakini natambua pia kuwa wengi wao wanakabiliwa na matatizo ya kifedha wakati huu , hii ikimaanisha kwamba lazima tuangalie njia zingine za kuchangisha fedha kukabili mahitaji ya haraka yaliyopo."

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi pamoja na serikali zote duniani kuimarisha mipango yao ya kukabiliana na majanga ili kupunguza athari yatakapotokea.