Ban apongeza utoaji matokeo katika uchaguzi wa Kyrgystan

2 Novemba 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wananchi wa Kyrgyzstan kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Bunge uliofanyika October 10.

Matokeo hayo ambayo yamefanyiwa tathmini waangalizi yamesifiwa kuwa hayakuwa na dosari yoyote. Ban amesema hali hiyo ni ya kutia matumaini na inafaa sasa kuundwa kwa serikali ambayo itahakikisha amani ya kudumu inakuwepo.

Uchaguzi huo uliofanyika miezi minne iliyopita baada ya kutokea kwa machafuko ya umwagaji damu baina ya makabila ya Kyrgyz na Uzbeks ambayo yaliathiri maisha ya mamilioni ya watu. Ban amemdhibitishia rais Kyrgyz Rosa Otunbaeva kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kutoa uungaji mkono wake ili kurejesha katika hali ya utengamao kwenye eneo hilo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter