Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia inajitahidi kuwawezesha wanawake kiuchumi:Tah

Liberia inajitahidi kuwawezesha wanawake kiuchumi:Tah

Waziri wa haki wa Liberia leo amesema nchi yake inafanya juhudi kubwa kuimarisha hali ya uchumi ya wanawake, hasa wakati huu kukiwa na tatizo kubwa la ajira.

(SAUTI YA CHRISTIANA TAH)

"Anasema mradi huu unatoa mafunzo ya ujuzi wa kiuchumi kwa wanawake na una lengo la kuimarisha uwezo wa wanawake wakulima na wafanya biashara, na zaidi ya hayo mabadiliko ya sheria yaliyofanywa na serikali yamesaidia kuinua hali ya uchumi ya wanawake nchini Liberia. Kwa mfano mabadiliko ya sheria ya mirathi, imeimarisha sana haki ya kumiliki mali kwa wanawake walioolewa katika sheria za kimila.