Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuunda jopo kusaidia upatikanaji amani Afghanstan

UM kuunda jopo kusaidia upatikanaji amani Afghanstan

Timu ya wawakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan imetangaza kuanzisha jopo la maalumu la wataalamu ambao watakuwa na kazi ya kuwasaidia viongozi waliochaguliwa hivi karibuni nchini humo wanaounda baraza la wawakilishi kwa ajili ya kusaidia kunakuwepo na amani ya kudumu.

Jopo hilo la wataalamu linalojulikana kama kundi la utoaji msaada litawajibika moja kwa moja kuanisha mipango na mikakati itayosaidia inazika vitendo vya kihasama na kupalilia amani ya kudumu.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Staffan de Mistura amesema kuwa hatua ya uundwaji wa jopo hili umekuja baada ya kufanyika majadiliano ya mashariano baina ya pande zote mbili.

Mistura amepongeza hatua ya uundwaji wa baraza la amani ngazi ya juu akisema kuwa litatoa msaada mkubwa wa kupatikana kwa amani ya kudumu kwenye eneo hilo.