Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa jamii za cyprus za Ugiriki na Uturuki kukutana na Ban

Viongozi wa jamii za cyprus za Ugiriki na Uturuki kukutana na Ban

Viongozi wa jamii za Cypriot za nchini Uturuki na Ugiriki wanatarajiwa kukutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon baadaye mwezi huu mjini New York Marekani kwa mazungumzo yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yenye lengo la kukiunganisha kisiwa hicho cha Mediterranean.

Kiongozi wa jamii ya Cypriot ya nchini Ugiriki Dimitris Christofias na mwenzake kutoka Uturuki Dervis Eroglu wamekuwa wakikutana kwa wakati fulani wakiwa na nia ya kuunganisha jamii hizo kulingana na azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Jamii hizo zitaungana chini ya serikali moja ya shirikisho huku kila moja ikiwa na jimbo lililo sawa. Mapema mwezi uliopita Ban aliwashauri viongozo hao wawili kuzingatia mazunguzo yao na kuongeza kasi ya mazunguzo hayo akisema kuwa yamekuwa yakijikokota katika siku za hivi karibuni.