Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yazindua njia 30 kwa siku 30 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

UNEP yazindua njia 30 kwa siku 30 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Kuanzia leo ambapo ni mwezi mmoja kabla ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mjini Cancun Mexico, shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linatoa utafiti kwenye mtandao kuonyesha kwamba suluhisho la matatizo la mabadiliko ya hali ya hewa lipo.

Lengo la UNEP kwa utafiti huo ni kuonyesha kwamba duniani kote kwa njia mbalimbali kuanzia mipango ya kijamii, hadi ya kimataifa , suluhu ipo ili kusaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na kuzisaidia nchi , jamii na biashara kuelekea kwenye matumizi madogo ya gesi ya cabon na kuchagiza ukuaji wa uchumi.

Baadhi ya mambo yaliyotajwa na UNEP ni mikopo kwa ajili ya matumizi ya nishati ya jua, utalii unaozingatia mazingira, kilimo cha hai, misitu ya Panama na Afrika itakuwa sehemu ya suluhisho pamoja na mpango wa UNEP wa njia 30 kwa siku 30 uliozinduliwa leo.