Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wamtaka waziri mkuu mpya wa Somalia kuunda serikali

UM wamtaka waziri mkuu mpya wa Somalia kuunda serikali

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amemtolea wito waziri mkuu mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi kuunda serikali ili kuendelea kukabili changamoto zinazolighubika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Dr Augustine Mahiga ambaye amempongeza pia waziri mkuu huyo baada ya kuthibitishwa na bunge na kuapishwa hapo jana , pia amemtia moyo wa kuendendeleza masuala yaliyosalia kabla ya kumalizika kipindi cha mpito cha serikali iliyoko madarakani hizi sasa. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Balozi Augustine Mahaiga amesema Abdullahi Mohamed anawajibika kuunda serikali yake hivi sasa ili ianze kutafakari namna ya kushughulikia matatizo yanayoendelea kuikabili nchi hiyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa hata hivyo ameelezea matumaini yake hasa kutokana na uungwaji mkono mkubwa unaotolewa toka kwa jumuiya za kimataifa. Ameeleza kuwa nchi za kienea ikiwemo IGAD zimetoa ishara njema kwa Waziri huyo mkuu mpya.

Bwana Mohamed aliapishwa hivi karibuni kushikwa wadhifa wa Waziri Mkuu wa Somalia kufuatia kujizulu kwa mtangulizi wake Omar Abdirashid Sharmarke.