UM na serikali ya Haiti wajiandaa kwa kimbunga Tomas

UM na serikali ya Haiti wajiandaa kwa kimbunga Tomas

Serikali ya Haiti, mashirika ya misaada na mpango wa Umoja wa Mataifa Haiti MINUSTAH wametayarisha mkakati wa kukabiliana na kimbunga Tomas kinachotarajiwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa takwimu kimbunga hicho kinahofiwa kitaathiri watu takribani laki tano. Pamoja na vifaa vya akiba vilivyopo msaada mwingine utakaohitajika ni mahema 150,000,katoni elfu 90 za sabuni, kasha elfu 90 za vifaa vya usafi, paketi 200,000 za Oral rehydration salt ambayo ni tiba ya kipundupindu na mahema makubwa 50 yatakayotumika kama vituo vya dharura vya matibabu.

Vifaa vingine ni radio za mawasiliano, msaada wa kiufundi, na vipaza sauti kwa ajili ya kuwatangazia watu tahadhari ya kimbunga hicho. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA ni Elizabeth Byers

(SAUTI YA ELIZABETH BYERS OCHA)