Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu 700 wajadili kuzuia kuunda silaha za nyuklia

Wataalamu 700 wajadili kuzuia kuunda silaha za nyuklia

Mjadala kuhusu changamoto zinazolikabili shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA katika uhufadhi wa vifaa vya nyuklia umeanza leo mjini Vienna Austria.

Mkutano huo utakaokamilika Novemba tano umekusanya pamoja wataalamu 700, wakiwemo wawakilishi wa nchi wanachama wa IAEA, sekta ya nyuklia, na wajumbe wa jumuiya ya kuzuia uzalishaji wa silaha za nyuklia. Mjadala huo unatoa fursa kwa washiriki kwa pamoja kutanabahi suluhu ya changamoto katika siku za usoni ili kuisaidia IAEA kufuatilia masuala ya nyuklia.

Nchi nyingi duniani zinatumia nyuklia kwa shughuli za amani, na ili kuhakikisha mipango hiyo ya nyuklia haitumiki vibaya IAEA imeweka mfumo maalumu wa makubaliani, na nchi 170 zimetia saini makubaliano hayo ambayo yataruhusu IAEA kukagua mitambo yake ya nyuklia. Herman Nackaert ni naiabu mkurugenzi wa IAEA.

(SAUTI HERMAN NACKAERTS)

Mada kuu zitakazojadiliwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za kimataifa za kutozalisha nyuklia, jukumu la nchi ambazo sio wanachama, kuangalia mitandao ya biashara na utandawazi wa taarifa na teknolojia ya nyuklia.