Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Ivory Coast umefanyika kwa amani kinachosubiriwa ni matokeo:UM

Uchaguzi Ivory Coast umefanyika kwa amani kinachosubiriwa ni matokeo:UM

Baada ya kuahirishwa zaidi ya mara tano hatimaye uchaguzi wa Ivory Coast umefanyika kwa amani na utulivu jana Jumapili.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza watu wa Ivory Coast kwa kutumia haki yako ya msingi na kupiga kura kwa amani kwenye uchauguzi huo wa Urais. Amesema huu ni uchaguzi muhimu kwa juhudi za kurejesha amani ya kudumu nchini Ivory Coast.

Sasa amezitaka pande zote na wagombea wote kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha amani na utulivu inatawala na wakubali matokeo yatakayotangazwa, na kama wana malalamiko wayawasilishe kwa kufuata sheria.

Matokeo ya wali yanatarajiwa Novemba tatu. Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini humo Y.J.Choi amesema ametiwa moyo na hatua hiyo ya mwanzo ya uchaguzi. Jayson Nyakundi na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)