Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kambi bado muhimu kwa waathiriwa wa mafuriko miezi mitatu baada ya mafuriko kuikumba Pakistan

Kambi bado muhimu kwa waathiriwa wa mafuriko miezi mitatu baada ya mafuriko kuikumba Pakistan

Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa takriban watu milioni 7 bado hawana makao miezi mitatu baada ya mafuriko kuikumba Pakistan.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa kuna ukosefu mkubwa wa makao katika mkoa wa Sindh baada ya nyumba milioni moja kuharibiwa. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa huenda hali ikawa mbaya kwa kuwa itawalazimu maelfu ya watu kusalia kambini wakati wa majira ya baridi.Adrian Edwards na msemaji wa UNHCR mjini Geneva

Clip George atasoma na kuandika clip

Nayo ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema kuwa hadi sasa ni msaada ni msaada wa dola milioni 759 uliotolewa kusadia waathiriwa kwa mafuriko nchini Pakistan.