Ban alaani kisa cha kushambuliwa kwa wafanyikazi wa mahakama inayoungwa mkono na UM nchini Lebanon

Ban alaani kisa cha kushambuliwa kwa wafanyikazi wa mahakama inayoungwa mkono na UM nchini Lebanon

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani kisa ambapo wafanyikazi wa mahakama inayoungwa mkono na UM iliyobuniwa kuwahukumu washukiwa wa mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri walishambuliwa na kukitaja kitendo hicho kama ambacho hakitakubalika.

Kwenye ripoti kupitia kwa msemaji wake Ban alisisitiza kuwa mahakama hiyo ni huru baada ya kubuniwa kwa ombi la serikali ya Lebanon akisema kuwa ni chombo muhimu cha kupata ukweli. Hii ni baada ya wachunguzi wawili kutoka kwa ofisi ya mwendesha mashataka wa mahakama hiyo pamoja na mkalimani wao waliokuwa wamehudhuria mkutano kwenye ofisi moja ya dakarati kama moja ya uchunguzi wao kushambuliwa na kundi la watu lililokuwa na hasira. Ban ametoa woto kwa pande husika kutoingilia kati majukumu ya mahakama hiyo.