Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 22,000 wazaliwa na virusi vya ukimwi nchini Kenya kila mwaka

Watoto 22,000 wazaliwa na virusi vya ukimwi nchini Kenya kila mwaka

Inakadiriwa kuwa watoto 22,000 wanaozaliwa nchi Kenya kila mwaka wanaambukizwa virusi vya ukimwi nchini Kenya.

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa kuzaliwa kwa idadi kubwa ya watoto walio na virusi vya ukimwi nchini Kenya kunasababishwa na wazazi walio na virusi hivyo kukosa kuhudhuria kliniki ambapo wanaweza kupewa matibabu ya kuzuia kumwambukizia mtoto virusi. Ili kukabiliana na hali hiyo shirika la UNICEF limeanzisha mpango mpya la kutoa madawa ya antiretroviral ambayo wanawake wajawazito wanaweza kutumia wakiwa nyumbani. Marixie Mercado ni kutoka shirika la UNICEF mjini Geneva:

(SAUTI YA MARIXIE MERCARDO)

UNICEF Linasema kuwa bila ya matibabu karibu nusu ya watoto wanaozaliwa wakiwa na virusi vya Ukimwi watakufa kabla ya kutimu umri wa miaka miwili. Mpango huo pia utapelekwa nchini Cameroon, Lesotho na Zambia.