Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka nchi za Chad na Afrika ya kati ziungwe mkono wakati MINURCAT ikijiandaa kuondoka

Ban ataka nchi za Chad na Afrika ya kati ziungwe mkono wakati MINURCAT ikijiandaa kuondoka

Wakati vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika nchi za Chad na Jamhuri ya Kati MINURCART vikiwa katika maandalizi ya kuondoka kwenye nchi hizo, Katibu Mkuu wa Umoja huo wa Mataifa ametia uzito haja ya kuziunga mkono nchi hizo ili ziweze kutatua matatizo yake zenyewe.

Bwana Ban Ki-moon amesema lazima nchi hizo ziungwe mkono na kupewa nafasi ya ili ziweze kusaka ufumbuzi kwenye changamoto zinahusika na masuala ya usalama pamoja misaada ya kibinadamu.

Kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kinachojulikana kama MINURCAT kilipelekwa kwa kuzingatia azimio la Baraza la usalama mnamo mwaka 2007 kwa shabaya ya kutoa ulinzi na kuhakikisha usalama wa raia kufuatia machafuko yaliyozuka baina ya nchi hizo mbili na mzozo mwingine ulioihusisha Sudan.

Kinatazamiwa kumaliza kazi yake mwishoni mwa mwaka huu kufuatia ombi lililowakilishwa na Serikali ya Chad kwa baraza la usalama.