Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu la UM lazingatia kazi za mahakama za dunia katika kutatua migogoro

Baraza kuu la UM lazingatia kazi za mahakama za dunia katika kutatua migogoro

Idadi kubwa ya nchi zinaitumia mahakama ya kimataifa ya haki ICJ kutatua mivutano. Hayo yamesemwa na Rais wa ICJ Hisashi Owada.

Akiwasilisha ripoti kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa amesema ongezeko la kesi ni dalili ya jinsi viongozi wa kisiasa duniani wanavyotambua umuhimu wa utawala wa sheria. Jaji Owada ameliambia baraza kuu kwamba hivi sasa kuna kesi 16 inazohusisha takribani nchi 30 tofauti.

(SAUTI YA JAJI OWADA)

Anasema bila shaka ni lazima isisitizwe kwamba umuhimu wa utawala wa sheria katika jumuiya ya sasa ya kimataifa unaongezeka kwa haraka dhidi ya mifumo inayosuasua ya utandawazi. Sitii chumvi kusema kwamba utawala wa sheria sasa unagusa kila nyanja ya shughuli za Umoja wa Mataifa.