Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watathimini athari za tsunami na volkano Indonesia

UM watathimini athari za tsunami na volkano Indonesia

Umoja wa Mataifa pamoja na washirika wake umeanza kuisadia Serikali ya Indonesia kufanya tathmini namna matukio ya tsunami na mlipuko wa volcano ilivyowaathiri wananchi wa eneo hilo.

Matukio hayo yamearifiwa kutokea mwanzoni mwa wiki hii. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wa huduma za usamaria wema OCHA, wamesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kwamba mamlaka nchini humo zilikuwa na uwezo wa kukabiliana na hali hiyo.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa na wale wa serikali ya Indonesia wameendelea kufanya tathmini yao juu ya tukio la tsunami, ambalo lilisababishwa na tetemeko la ardhi lenye kipimo cha ritcher 7.2 Watu 154 tayari wamethibitika kupoteza maisha na wengine 400 bado hawajulikani waliko. Nyumba 179 ziliharibiwa vibaya wakati nyingine 300 zikinusurika.