Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vitisho havitukatazi kutafuta ukweli wakifo cha Hariri:UM

Vitisho havitukatazi kutafuta ukweli wakifo cha Hariri:UM

Mahakama moja inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuendesha kesi dhidi ya mauwaji ya kiongozi wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri imelaani vikali shambulio kwa watumishi wake kadhaa na ikaonya kwamba vitendo vya namna hivyo havitaitishia mahakama hiyo kuendelea na kazi zake.

Maafisa wa Umoja huo wa Mataifa wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo kimoja cha kazi kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi Mjini Beirut, walivamiwa na kundi la watu kwa nia ya kutaka kuwazuru. Maafisa hao watatu walipoteza baadhi ya vitendea kazi vyao.

Katika taarifa yake juu ya tukio hilo, Mahakama inayoendesha kesi hiyo yenye makao yake Mjini The Hague imesema kuwa, matukio kama hayo hayawezi kuwavunja moyo wasitishe juhudi zao za kusaka ukweli. Mahakama hiyo imesema kuwa itaendelea kuendesha mambo yake kwa uwazi na ukweli na wala haitatishika na kitisho chochote.