Skip to main content

Maeneo yanayolindwa Afrika, Asia kupata ufadhili:UNEP

Maeneo yanayolindwa Afrika, Asia kupata ufadhili:UNEP

Zaidi ya maeneo 15 yanayolindwa yakiwemo ya watawa nchini Mauritania na makao ya nyani afahamikaye kama Orangutangu, Chui na Ndovu yaliyo katika kisiwa cha Sumatra yatapokea dola milioni 6.8 kugharamia jitihada za kulinda maeneo hayo.

Hii ni baada ya serikali ya Hispania , shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na lile la LifeWeb kutangaza ushirikiano wa kuyalinda maeneo hayo kwenye mkutano kuhusu bayo anuai unaondaliwa mjini Nagoya nchini Japan.

Ushirikiano huo unaofadhili nchi masikini na zile zinazoendelea una lengo la kutoa manufaa kwa bayo anuai lakini pia kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo yanayolindwa. Waziri wa mabadiliko ya hewa wa Hispania Teresa Ribera anasema kuwa changamoto iliyopo ni kuhakikisha kuwa zaidi ya maeneo 100,000 kote duniani yamepata usimamizi mwema ili kuwafaidi wenyeji.