Angola yawatimua wakimbizi 150 wa DRC:OCHA

28 Oktoba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema taarifa za karibuni za kutimuliwa wakimbizi zaidi ya 150 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Angola huenda likazua wimbi jipya la kurejeshwa kwa nguvu wakimbizi katika nchi hizo mbili.

OCHA inasema kwa mujibu wa taarifa ilizopokea wakimbizi hao wakiwemo wanawake 30 wanaodaiwa kubakwa mara kadhaa wamewasili mjini tembo jimbo la Bandundu Magharibi mwa Congo wakidai kufukuzwa na serikali ya Angola Jayson Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Nayo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanaripoti kuwa wakati wa kufukuzwa huku wanaume wawili waliuawa na wanawake 30 kubakwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa serikali ya DRC imedhibitisha kuwa raia wake 40 wamewasili katika eneo la Kasongo-Lunda baada kusemekana kuwa walilazimishwa kuondoka nchini Angola.

Msemaji wa shirika la OCHA Maurizio Giuliano anasema kuwa hata kama idadi ya waliofukuzwa ni ndogo huenda ikawa mwanzo wa kufukuzwa kwa wengi. Mwaka uliopita raia 160 wa DRC walifukuzwa kutoka Angola huku raia 51,000 wa Angola wakifukuzwa kutoka DRC.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud