Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndege ya kwanza ya misaada ya UNHCR imewasili Benin

Ndege ya kwanza ya misaada ya UNHCR imewasili Benin

Ndege ya kwanza ya misaada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imewasili mjini Cotonou Benin mapema leo asubuhi.

Ndege hiyo kutoka Ubelgiji imebeba mahema 1500 yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye kituo cha akiba cha shirika hilo mjini Copenhagen. Mahema hayo yatawasaidia wanaohitaji msaada wa haraka wa malazi baada ya kuathirika na mafuriko makubwa.

Wataalamu wa masuala ya kiufundi wa UNHCR waliopelekwa Benini siku ya Jumatatu wanasema ndege hiyo imewasili kwenye uwanja wa ndege wa Cotonou na ndege nyingine iliyosheheni msaada mbalimbali ikiwemo mahema zaidi inatarajiwa kuwasili kesho Ijumaa watu takribani 680,000 wameathirika na mafuriko nchini humo. Bennin ni moja kati ya nchi karibu saba za Afrika ya Magharibi zilizokumbwa na mafuriko hivi karibuni.