Skip to main content

Ban amesikitishwa na habari za kifo cha Nestor Kirchner

Ban amesikitishwa na habari za kifo cha Nestor Kirchner

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha Nestor Kirchner.

Bwana Kirchner alikuwa katibu mkuu mtendaji wa muungano wa mataifa ya Amerika ya Kusini UNASUR, Rais wa zamani wa Argentina na alikuwa naibu wa sasa wa bunge la Argentina. Ban amesema bwana Kuichner ambaye alikuwa pia mume wa Rais wa sasa wa Argentina Bi Cristina Fernandez de Kurchner alikuwa rafiki wa Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kuwa alikuwa kiongozi wa kitaifa na kimataifa aliyeamini masuala ya usawa na ushirikiano. Ban ametoa salamu za rambirambi kwa Rais Christina Fernandez na familia yake, pia kwa serikali na watu wote wa Argentina.