Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi wanachama wa UM lazima zishiriki vita dhidi ya ugaidi

Nchi wanachama wa UM lazima zishiriki vita dhidi ya ugaidi

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa juu ya uhalifu wa kimataifa amesema kuwa ugaidi umeendelea kuwa kitisho kikubwa lakini hata hivyo hauwezi kuleta mkwamo wowote katika kufikia amani ya dunia.

Akizungumza Mjini New York, Martin Scheinin amesema kuwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapaswa kusaidiana kukabilia vitendo vya kigaidi na isidhaniwe kuwa ni jukumu la Baraza la Usalama ambalo limepewe mamlaka ya kufanya maamuzi ya aiana mbalimbali.

Hadi sasa nchi 172 zimesaini itifaki ya Umoja wa Mataifa inayotaka kuwepo kwa utashi wa pamoja wa kukabiliana na vitendo vya kigaidi.