Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaanza kugawa mbegu za ngano nchini Pakistan

FAO yaanza kugawa mbegu za ngano nchini Pakistan

Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limeanza mradi mkubwa wa usambazaji wa mbegu za ngano kwa wakulima nchini Pakistan.

FAO inagawa mbegu hizo ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa chakula katika siku za usoni baada ya nchi hiyo kukumbwa na mafuriko makubwa. Kwa mujibu wa FAO mradi huo utazinufaisha familia takribani milioni tano za wakulima nchini Pakistan. George Njogopa na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mbegu hizo zinatazamiwa kuanza kutumia wakati msimu wa kilimo ambao ulitarajiwa kukoma mwezi wa Disemba lakini shughuli hizo zitaendelea licha ya hali mbaya ya eneo hilo iliyosababishwa na mafuriko makubwa ya hivi karibuni.

Hatua hiyo ya usambazaji wa mbegu ni muhimu ili kufufua upya zao hilo la ngano ambalo liliharibiwa vibaya na mafuriko hayo. Karibu tani 500,000 mpaka 600,000 zilitoweka na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.