Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uweze wa uzalishaji katika nchi masikini ni muhimu:UNCTAD

Uweze wa uzalishaji katika nchi masikini ni muhimu:UNCTAD

UNCTAD inasema matumizi ya huduma na bidhaa zinazozalishwa nchini kunasaidia kutoa fursa za kazi zinazolipa vizuri na kuboresha kiwango cha maisha ya watu.

UNCTAD imeyasema hayol eo katika mwanzo wa mkutano wa siku tatu mjini Geneva Switzerland unaojadili nini kifanyike kuzisaidia nchi 49 masikini kabisa duniani kuimarisha uwezo wake wa uzalishaji . Mkutano huo ni moja ya matukio mbalimbali yaliyoandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutoa mawazo ya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi masikini utakaofanyika kuanzia tarehe 30 May hadi Juni 3 2011 nchini Uturuki.

Mada ya mkutano ulioanza leo kujenga uwezo wa uzalishajikatika nchi zisizo na maendeleo LDC's imetokana na utafiti na ushauri wa sera za UNCTAD zisemazo umasikini unaweza kupunguzwa kwa kupiga hatua katika masuala ya uchumi. Supachai Panitchpakdi ni katibu mkuu wa UNCTAD

(SAUTI YA SUPACHAI)

Washiriki wa mkutano huo wataangalia pia jinsi gani kujenga uwezo wa uzalishaji kutakavyoathiri mfumo wa sera za kitaifa ili kuchagiza maendeleo na kupunguza umasikini katika nchi hizo pia mfumo wa msaada wa kimataifa kutoka kwa washirika wa nchi hizo. Nchi zisizoendelea ni zile zenye umasikini uliokithiri, matatizo ya afya ikiwemo utapia mlo, zinazotegemea kilimo cha kizamani na misaada kutoka nje.