Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya afya Haiti ilishtukizwa na kipindupindu:WHO

Sekta ya afya Haiti ilishtukizwa na kipindupindu:WHO

Sekta ya huduma za afya nchi Haiti haikuwa imejiandaa kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu limesema shirika la afya duniani WHO.

Limesema mlipuko wa ugonjwa huo umewashtukiza bila kutarajia wafanyakazi wa afya wa kitaifa na kimataifa jambo ambalo huenda limechangia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo . Visa 3769 vya kipindupindu vimeripotiwa na watu 289 wameshafariki dunia.

Dr Claire Chaignat kutoka WHO anasema idadi ya vifo inapungua kutokana na kuongeza juhudi katika matibabu na watu kupata ufahamu kuhusu ugonjwa huo. Haiti haijakuwa na mlipuko wa kipindupindu kwa zaidi ya miaka 100.

(SAUTI YA CLAIRE CHAIGNAT)

WHO inasema kipindupindu huenda kikakita mizizi Haiti kutokana na mazingira machafu na visa vingine kuripotiwa muda mrefu baada ya mlipuko wa sasa kudhibitiwa.