Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani uvamizi dhidi ya walinda amani wa MONUSCO

UM walaani uvamizi dhidi ya walinda amani wa MONUSCO

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amelaani vikali vitendo vya uvamizi vilivyofanywa dhidi ya askari wa amani wa Umoja wa Mataifa walioko katika eneo tete la mashariki mwa nchi hiyo.

Roger Meece amesema kuwa tukio hilo ambalo limetokea mwishoni mwa wiki linatoa tasfri kuwa bado kunahitajika uungwaji mkono toka jumuiya za kimataifa kuisaidia Serikali ya Congo.

Kundi hilo la waasi likiwa na silaha mbalimbali lilisonga mbele hadi kwenye ngome ya askari wa kulinda amani na hata lilipopewa ishara ya kurejea nyuma, halikutii agizo hilo. Duru zaidi zinasema kuwa kwenye prukushani hizo waasi nane walipoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa.