Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yaitaka Kenya kumkamata Rais Al Bashiri akiwasili

ICC yaitaka Kenya kumkamata Rais Al Bashiri akiwasili

Kitengo cha kesi cha mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC imeiomba serikali ya Kenya kuiarifu mahakama hiyo sio zaidi ya tarehe 29 Oktoba kuhsu tatizo lolote litakalozuia kumkamata au kujisalimisha kwa Rais Omar Al Bashir wa Sudan.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais Al Bashir atasafiri kwenda nchini Kenya mwishoni mwa wiki kuhudhuria mkutano wa IGAD uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba.

Mahakama ya ICC inataka Rais Bashir akamatwe na kukabidhiwa kwa mahakama hiyo ikiwa ni kutimiza wajibu wa Kenya kuwa nchi mwanachama wa kuridhia mkataba wa Roma uliotiwa saini Juni Mosi 2005. Bashir anatakiwa na mahakama hiyo kujibu mashitaka mbalimbali yakiwemo ya uhalifu wa kivita na ukatili dhidi ya ubinadamu.