Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 60,000 wasambaratishwa na mapigano mapya Somalia

Watu 60,000 wasambaratishwa na mapigano mapya Somalia

Watu wapatao elfu 60 wamesambaratishwa na machafuko mapya nchi Somalia kwenye mji wa Beled Hawo Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mapigano hayo kati ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali ya mpito yamekatili maisha ya watu 10. Chanzo cha mapigano hayo ni kugombea udhibiti wa mji huo.

Andrej Mahecic msemaji wa UNHCR anasema watu elfu 5000 wamekimbia mapigano hayo na tayari wameshaandiskiwa kwenye mpaka wa Kenya , ingawa wakimbizi wapatao 20,000 wanaaminika kuvuka mpaka na kuingia Kenya.

(SAUTI ANDREJ MAHECIC)

UNHCR inasema hali ya wasiwasi imetanda katika mji huo na watu wengi zaidi wanatarajiwa kukimbia, kwani kumekuwa na taarifa kwamba kundi la waasi la Al-Shabaab linajipanga upya kufanya mashambulizi ili kuchukua udhibiti wa mji huo.