Skip to main content

MUNUSCO yasherehekea miaka 65 ya UM mjini Ben DR Congo

MUNUSCO yasherehekea miaka 65 ya UM mjini Ben DR Congo

Umoja wa Mataifa umeadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa tarehe 24 Oktober 1945. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na dunia kwa ujumla imeungana na Umoja wa Mataifa katika shamrashamra hizo hasa kwa kutambua umuhimu wa chombo hiki cha kimataifa.

Mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban ki-moon amesema wanaongeza juhudi za kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hasa masuala ya usalama, umasikini, silaha za nyuklia, mabadiliko ya hali ya hewa na kuhakikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanatimizwa.

Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mjini Ben wafanyakazi wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wameungana na wananchi kusherehekea leo jumatatu siku hiyo ya Umoja wa Mataifa na mwandishi wa habari wa eneo hilo Mseke Dide amezungumza na mkuu wa ofisi ya MONUSCo Beni Ahmed Sharif kuhusu hafla hiyo