Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini ya kukua kwa uchumi Afrika:IMF

Kuna matumaini ya kukua kwa uchumi Afrika:IMF

Shirika la fedha duniani IMF linasema nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara zitafaidika na kukuwa kwa uchumi katika sekta mbalimbali.

Katika takwimu zake za karibuni kuhusu uchumi katika eneo hilo IMF imesema Afrika huenda ikashuhudia mahitaji makubwa ya ndani yakienda sambamba na ongezeko la usafirishaji bidhaa nje hali ambayo itafufua uchumi wa nchi hizo baada ya mdororo.

Lakini mkuu wa idara ya Afrika katika IMF Antoinette Sayeh amesema nchi za Afrika bado zinahitaji kujikita katika kuweka mazingira bora ya biashra. Ameongeza kuwa bado inachukua muda mrefu sana katika baadhi ya nchi kuweka mazingira mpya ya biashara jambo ambalo linaweza kuboreshwa katika baadhi ya nchi.

Amesema lazima kuwe na uwiano baina ya bidhaa zinazoingia na zile zinazotoka katika nchi hizo, na uwekezaji wa ndani na nje ni muhimu ili kuzifanya sekta binafsi kuwekeza kwa muda mrefu katika uchumi wa Afrika, kwani hiyo ndio changamoto ya siku zinajazo.