Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast iko tayari kwa uchaguzi wa Rais:UM

Ivory Coast iko tayari kwa uchaguzi wa Rais:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast amesema nchi hiyo iko tayari kufanya uchaguzi wa Rais uliosubiriwa kwa muda mrefu tarehe 31 ya mwezi huu.

Uchaguzi huo ni sehemu ya makubaliano yaliyoafikiwa 2007 ili kuunganisha nchi hiyo iliyogawika mapande mawili kutokana na vita zilivyozuka 2002. Mwakilishi huyo Choi Young-Jin amesema kwamba tayari kuna tarehe maalumu iliyowekwa ya kutangaza matokeo ya awali na ya kutangazwa matokeo rasmi.

Ameongeza kuwa hata hivyo kuna changamoto kadhaa za kiufundi na kisiasa zilizobainika, lakini kwa bahati nzuri wamezipatia ufumbuzi zote.  Kwa sasa amesema haoni kiwazo chochote kikubwa hadi Oktoba 31. Hivyo amesema siku hiyo itakuwa ya kihistoria na uchaguzi utafanyika tarehe hiyo.