Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea kufaidika na muongozo wa kusafirisha bidhaa:UNIDO

Nchi zinazoendelea kufaidika na muongozo wa kusafirisha bidhaa:UNIDO

Wasafirishaji bidhaa nje katika nchi zinazoendelea sasa wataweza kufaidika na muongozo mpya uliotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO.

Muongozo huo ni wa kusaidia kuweka viwango binafsi kwa bidhaa kama nguo, viatu na samani ili kuimarisha uwezekano wa kupata masoko ya kimataifa.

Muongozo huo uliochapishwa kama kitabu na UNIDO na kupewa kichwa Kufanya viwango binafsi vikusaidie" unaainisha thamani ya biashara, taratibu, sheria , misingi na kanuni ambazo zinachukuliwa kama muhimu sana kwa kuchagiza maendeleo ya jamii na kulinda mazingira katika soko la kimataifa.

Kwa mujibu wa UNIDO kuna kanuni zaidi ya 1000 za kuendesha na kuhimili mfumo wa biashara, lakini makampuni mengi katika nchi zinazoendelea hayana taarifa za kutosha kuhusu kanuni hizo.