Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Asia-Pacific zakutana katika maandalizi ya G-20:UM

Nchi za Asia-Pacific zakutana katika maandalizi ya G-20:UM

Zaidi ya nchi 24 za Asia-Pacific zimekutana kwa ajili ya mkutano wa Umoja wa Mataida ulioanza leo kujadili masuala nyeti yahusuyo ukuaji wa uchumi katika maandalizi ya mkutano wa G20 mwezi ujao.

Mkutano huo wa siku mbili wa majadiliano mjini Bankok umeandaliwa na tume ya uchumi na jamii ya Umoja wa Mataifa kwa nchi za Asia na Pacific ESCAP, unataka kuratibu sauti moja ya kanda nzima na kujadili mtazamo tofauti na ule wa G20.

Washiriki wanatarajiwa kuafikiana jinsi gani wapunguze pengo la maendeleo lililopo, matatizo ya fedha na mabadiliko ya utawala wa kimataifa. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa ESCAP Noeleen Heyzer mkutano wa G20 utakaofanyika Novemba 11-12 mjini Seoul Jamhuri ya Korea utakumbukwa kwa kuleta maendeleo kwenye ajenda ya G20 kwa mara ya kwanza.

Akihutubia katika mwanzo wa mkutano wa Bankok Bi Heyzer amesema changamoto zilizoletwa na matatizo ya uchumi ni fursa nzuri ya kuchagiza maendeleo yatakayojumuisha wote kwenye kanda hiyo ambayo ina watu masikini milioni 950 ambao wanakabiliwa na pengo kubwa kati ya walionacho na wasio nacho.

Ameongeza kuwa ni muhimu kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015 ili kuinua hali ya amisha ya watu bilioni moja wa kanda hiyo na kuwatoa katika umasikini.