Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera za umma zinaweza kuzuia magonjwa sugu:WHO

Sera za umma zinaweza kuzuia magonjwa sugu:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa magonjwa yasiyo na tiba kama vile magonjwa ya moyo, saratani , kisukari na kiharusi ndiyo yanaachangia asilimia 60 ya vifo duniani.

Kati ya watu milioni 35 waliokufa kutokana na magonjwa hayo mwaka 2005 nusu yao walikuwa nchini ya miaka 70 huku nusu wakiwa ni wanawake.

Kulingana na WHO magonjwa haya ndiyo chanzo kikubwa cha umaskini na kizuizi cha maendedeleo kwa nchi nyingi wakati ambapo asilimia 80 ya vifo vinavyotokana na magonjwa vikishuhudiwa kwenye nchi maskini.