Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi kwenye ofisi za UM Afghanistan

Ban alaani mashambulizi kwenye ofisi za UM Afghanistan

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye makao ya Umoja wa Mataifa mjini Herat nchini Afghanistan.

Msemaji wake Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa unaendesha uchunguzi kuhusu shambulizi hilo ambapo washambulizi kadha waliuawa. Ban amesema kuwa hatua za haraka zilizochukuliwa na walinda usalama nchini Afghanistan ziliokoa maisha ya wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kuwa UM utaendelea kusalia na kuendesha shughuli zake katika eneo la Herat kuwasaidia wenyeji na kuusadia utawala wa Afghanistan. Hakuna mfanyikazi wa UM aliyejeruhiwa kwenye shambulizi hilo isipokuwa walinzi wa makao hayo.