Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

kipindupindu kimeenza kudhibitiwa Haiti:OCHA

kipindupindu kimeenza kudhibitiwa Haiti:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa hadi sasa watu 254 wameaga dunia nchini Haiti kutokana na ugonjwa wa kipindupindu na wengine 3,015 kuambukizwa ugonjwa huo.

Hata hivyo UM kwa ushirikiano na serikali unapanga kuwahudumia waathiriwa. Pia misaada unaendelea kutolewa wakati ambapo serikali , mashirika ya Umoja wa Mataiofa na yasiyokuwa ya kiserikali wanaendelea kutoa usaidizi katika maeneo yaliyoathirika.

Hata hivyo visa vya kusambaa kwa gonjwa huo kwa sasa ni vichache ikilinganishwa na wakati uliporipotiwa mara ya kwanza.Serikali ya Haiti , Umoja wa Mataifa wanafanya wawezalo kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo. Daniel Epstine ni afisa wa habari wa shirika la kimataifa la afya PAHO.

(SAUTI YA DANIEL EPSTINE)