Skip to main content

Mkataba wa bayo-anuai kugharimu dola bilioni 30 kwa mwaka

Mkataba wa bayo-anuai kugharimu dola bilioni 30 kwa mwaka

Awamu ya pili ya mkutano wa kumi wa nchi wanachama wa makubaliono ya balojia anuai kwa sasa unaendelea kwenye mji wa Nagoya nchini Japan.

Serikali zinakutana kujadili maendeleo yaliyopigwa baada ya makubaliono ya mwaka 2002. Mkutano huu unaandaliwa wakati wa mwaka wa kimataifa wa baolojia anuai kama ilivyopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa. David Ainsworth ni msemaji wa mkutano huo.

(SAUTI YA DAVID AINSWORTH)

Mkataba huo umeelezwa  kwamba utagharimu dola bilioni 30 kwa mwaka ili kuweza kutekeleza makubalino hayo yaliyofikiwa kuhusu bayo-anuai.