Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atuma rambirambi kufuatia kifo cha waziri mkuu Barbados

Ban atuma rambirambi kufuatia kifo cha waziri mkuu Barbados

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa Barbados, David Thompson, na kumwelezea kuwa ni mtu aliyewajibika kulinda demokrasia na kusuma mbele hadhi ya Umoja wa Mataifa.

Bwana Thompson aliyaaga dunia mwishoni mwa wiki, alikuwa mjumbe wa ngazi ya juu katika jopo linaloshughulikia masuala ya dunia, yenye majukumu ya kuhakikisha inakabiliana na masuala ya mbalimbali kama kukabiliana na umaskini, kuweka mazingira endelevu na rafiki kwa ukuaji uchumi na mabadiliko ya tabia nchi.

Katibu Mkuu Ban ametuma salamu zake za rambirambi kwa ndugu na jamaa pamoja na serikali ya Barbados na watu wake.