Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wafuatilia mpango wa kuwapa vitabu maalumu wasioona

UM wafuatilia mpango wa kuwapa vitabu maalumu wasioona

Umoja wa Mataifa upo mbioni kutekeleza mpango ambao utashuhudia jamii ya watu wenye ulemavu wa kuona wakianza kufaidika na usomaji wa vitabu kupitia mkakati mpya wa uchapishaji vitabu.

Hatua hiyo imetangazwa na Umoja wa Mataifa kupitia jumuiya yake inayohusika na masuala ya kitaaluma WIPO, ambayo inakutana huko New Delhi India.  Mpango huo utaweka viashirio maalumu kwenye machapisho yatayowawezesha watu wenye ulemavu wa kuona kuweza kusoma bila shaka yoyote.

Vitabu vitakavyochapishwa kwenye mpango huo vinatazamiwa kusambazwa katika maktaba mbalimbali. Katika kukamilusha mpango huo WIPO,imeungana na taasisi nyingine mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya wasioona duniani, mashirika ya kirai na chama cha kimataifa cha wachapishaji vitabu.