Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muungano wa Afrika (AU) wataka msaada wa UM kuinusuru Somalia

Muungano wa Afrika (AU) wataka msaada wa UM kuinusuru Somalia

Hali ya usalama nchini Somalia bado ni tete, huku mamilioni ya watu wakiendelea kuwa wakimbizi wanaotegemea msaada wa kitaifa na kimataifa ili kuishi.

Nchi jirani pia zimeingiwa hofu kutokana na ukweli kwamba wanamganbo wa Kiislam wa Al-Shabab wanatafuta nguvu za ziada kutoka nje kwa lengo la kuitoa madarakani serikali ya mpito. sasa muungano wa afrika umelivalia njuga suala la Somalia na umelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutoa msaada wa ghali na mali ili vikosi vya kulinda amani vya muungano wa afrika Somalia vifanikishe azma ya kuleta amani Somalia.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Dr augustine Mahiga amemweleza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha kuwa ombi hilo lisipotekelezwa basi Somalia itaishia mikononi mwa magaidi. Wasikilize