Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM aliyezuru Haiti apongeza shughuli za misaada

Mjumbe wa UM aliyezuru Haiti apongeza shughuli za misaada

Hali ya usambazaji misaada ya kiutu nchini Haiti iliyokumbwa na tetemeko la ardhi ni ya kuridhisha kwa kiwango kikubwa, lakini hata hivyo jumuiya za kimataifa zitapaswa kuendelea kuhudumu hadi mwa 2011.

Hayo ni mwa mujibu wa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Bi Catherine Bragg ambaye amekamilisha ziara yake iliyolenga kufanya tathmini namna hali ya utoaji misaada inavyoendelea. Bi Bragg amesema kuwa kazi iliyokuwa ikifanywa na mashirika ya usamaria mwema kwa kushirikiana na serikali ya Haiti ni ya kupigiwa mfano kwani imeweza kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi.

Watu zaidi milioni 1 walifikiwa na huduma ya maji iliyokuwa ikitolewa kila siku, huku watu wengine milioni 4.3 wamepatiwa huduma ya chakula. Katika ziara yake hiyo Bi Bragg alitembelea kambi maalumu inayoendelea kuhifadhi watu zaidi ya milioni 1 ambao nyumba zao ziliharibiwa na tetemeko hilo.