Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM aendelea na ushawishi Sahara Magharibi

Mjumbe wa UM aendelea na ushawishi Sahara Magharibi

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye anahusika na mzozo wa Sahara Magharibi, ameendelea kuwa na mazungumzo na maafisa wa ngazi za juu kwenye eneo hilo, mnamo wakati kukisubiriwa kuanza kwa majadiliano mengine yenye shabaya ya kutanzua mvutano huo.

Morocco na eneo la Polisario iliingia kwenye mzozo kwa mara ya kwanza mwaka 1976 wakati Hispania ilipokomesha kipindi chake cha ukoloni.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa Christopher Ross tayari amekuwa na mazungumzo na maafisa wa ngazi wa juu wa Frente Polisario akiwasihi wakubali kurejea kwenye meza ya mazunguzmo ili kutanzua mzozo huo. Alielekea pia Algeria kwa shabaha hiyo hiyo ya kusaka ushawishi wa uungwaji mkono.

Anatazamiwa pia kuelekea Nouakchott, Mauritania na baadaye atakamilisha mzunguko wake huko Rabat, Morocco kwenyewe, kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuanza mazungumzo ya usakaji aman mwezi ujao.