Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ya Magharibi yanaendelea kughubikwa na mafuriko

Afrika ya Magharibi yanaendelea kughubikwa na mafuriko

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR litaanza kusafirisha misaada kwenda nchini Benin baada ya nchi hiyo kukumbwa na mafuro ambayo serikali na Umoja wa Mataifa wanakadiria kuwa yamewaathiri watu 680,000.

UNHCR inasema kuwa umeombwa kutoa misaada ya dharura kwa watu waliopoteza makwao katika maeneo ya kusini mwa nchi hata kama wajibu wake ni kuwashughulia wakimbizi 7300 nchini Benin.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA ni kuwa mafuriko yamekuwa yakishuhudiwa kwenye nchi nyingi za Afrika Mashariki ambapo zaidi ya watu milioni 1.5 wameathirika na vifo vingi kutokea. Elizabeth Byres ni msemaji wa shirika la OCHA

(SAUTI YA ELIZABETH BYRES)